FAIDA YA MATUMIZI YA TENDE KATIKA KUONGEZA KINGA YA MWILI NA TENDE

TENDE ni chakula chenye hali ya juu ya sukari na huliwa zikiwa mbichi au mbivu. Katika kila gramu 100 (100gm) mna lishe kwa asilimia ifuatayo:-

Moisture (Unyevunyevu)
15.3 %

Protein (hamirojo)
2.5%

Fat (mafuta)
0.4%

Carbohydrate (wanga)
75.8%

Fibre (kambakamba)
4%

Mineral matter (madini)
2.1 %
Baada ya funga ya muda mrefu kuanzia alfajiri hadi
jioni (magharibi) ni bora kufungua saumu yako kwa
kuanza kula tende kwa sababu ni chakula chepesi na husagwa tumboni kwa urahisi. Baada ya huleta nguvu mwilini haraka na pia hulipa
tumbo nguvu ya kusaga vyakula vitakavyofuatia baadae. Tende hutofautiana
katika ubora kutokana na kutegemea zinatoka nchi
gani. Pia hutegemea ikiwa tende hizo ni mpya kutoka shambani au ni za mavuno ya zamani.
Tende bora zaidi huwa na faida
nyingi za kitiba lakini bei yake ni ghali na tende ya hali ya chini na ya zamani kuvunwa bei yake ni
rahisi ukilinganisha na tende mpya lakini faida yake kimatibabu ni ndogo zaidi. Mimi kama Daktari nashauri watumiaji wa tende watumie
tende yenye kiwango cha juu ili wapate faida ya kitiba.
Pia ni changamoto kwa wafanya biashara ya tende watuletee na kutuuzia tende zenye ubora zaidi. Aidha wanunuzi nao wanunue tende zenye ubora wasijali ughali wa bei bali wajali ubora.

Lengo hapa ni kuelimisha jamii wala sio kuharibu biashara ya mtu. Nawahimiza tutumie tende katika miezi yote na wala si mwezi wa Ramadhani tu; na wale wasiokuwa Waislamu nawafahamisha kuwa tende si chakula cha Waislamu pekee bali ni cha watu wote.

FAIDA ZA TENDE KITIBA
1) Kifua, Mafua, Pumu: Saga kiasi cha tende kwenye blenda pamoja na asali na samli safi ya ng’ombe kisha changanya ndani yake kijiko kimoja cha chakula cha unga wa habbat
sauda na tangawizi.

Matumizi: Kula vijiko viwili vikubwa asubuhi na jioni.

2) Kutopata choo:- Tengeneza juisi ya tende na maji
au maziwa, kunywa glasi moja asubuhi na jioni.
3) Kuipa mishipa ya fahamu nguvu na kuimarisha

kumbukumbu:- Kula tende mara kwa mara huongeza kumbukumbu na fahamu.

4) Ni dawa ya kurejesha heshima nyumbani (Mujarrab):-
Huongeza kisu makali. Chukua tende kilo uondoe mbegu zakena saga ndani ya brenda pamoja na maziwa ya ng’ombe ongeza ndani yake kijiko kimoja cha unga wa uwatu na hulinjan ya unga.

Matumizi: Kunywa glasi moja asubuhi na jioni kila siku.

5) Mwanamke anaenyonyesha:- Kunywa kila siku asubuhi na jioni mchanganyiko wa Tende,
maziwa na uwatu.

6) Ukavu au kukauka kwa
mdomo na koo:- Kunywa juisi ya mchanganyiko wa
tende na maji asubuhi na jioni, hulainisha mdomo na
koo.

7) Sperms Additive:-
Huu ni mchanganyiko maalum wa madawa ya Kiarabu yaliyochanganywa na tende na maziwa ya moto ili kuongeza au kuzidisha sperms (yaani manii) kwa wale ambao wanahisi kuwa sperms (manii) ni chache au kuna
udhaifu. Ikiwa hupati mtoto nenda ukapime hospitalini sperms zako, kipimo hiki kinaitwa Sperms Counts au Sperms Analysis.
Ikiwa ni chache au dhaifu itabidi
uongeze kwa kutumia dawa hii ya Sperms Additive.

HITIMISHO Baada ya kuona au kuelimika kuhusu faida za tende, nawashauri watu wote tuendelee
kutumia tende hata baada ya mwezi wa Ramadhani sababu ndani yake mna lishe na faida kubwa za kitiba.

Comments

Popular posts from this blog

FIRST AID : UMUHIMU WAKE KATIKA MAISHA YA KILA SIKU

DOES SKIN CREAMS BLEACH THE SKIN, AND WHAT WOULD YOU RECOMMEND FOR ACNE SCARS ON THE FACE AND CHEST?