Posts

Showing posts from August, 2012

IT KEEPS YOUR SKIN BEUTIFUL!

Image
Pineapple contains enzymes that makes skin elastic, improves skin hydration, and remove demaged and dead cells. Thus it helps us achieve a clear and glowing complexion The enzymes in pineapples also fight free-radical demage and can reduce age spots and fine lines

FEW TRICKS TO TAKE YOUR MEDICATIONS CORRECTLY

Image
Pharmacists in hospitals and health systems play an important role in preventing medication errors. To make sure you use medicines safely and effectively, FeliRx Pharmaceuticals (0654408562) recommends that you: (1) Keep a list of all medications that you take (prescribed drugs, nonprescription medicines, herbal supplements, home remedies, and medical foods) and medicines that you cannot take due to allergic reactions, and share those with your doctor or pharmacist. (2.) Tell your health care provider (0654408562)how you actually take your medication, especially if this is different from the originally prescribed directions. Learn the names of the drug products that are prescribed and given to you, as well as their dosage strength and schedules. Ask if you should avoid certain foods, beverages, other medicines, or activities while you are taking the drug. Ask for any written information available on the drug product. Question anything you don't understand or that doesn...

JE, NI KWELI MATANGO NI DAWA?

Image
MATANGO si matunda mageni katika jamii ya Watanzania kwani hulimwa katika mikoa mbalimbali na mengine kuagizwa kutoka nchi za nje, hivyo kufanya upatikanaji wake uwe mzuri katika masoko ya ndani. Kihistoria, asili ya matango ni bara la Asia, hasa nchini India. Na matango yalianza kulimwa huko Asia zaidi ya miaka 3000 na baadae zao hilo kusambaa na kupokowa vizuri na nchi za magharibi hasa Ufaransa katika karne ya tisa. Baadae Uingereza na Marekani walianza kulima zao hilo katika karne ya 14 na 16. Matango yana uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali na kwa njia rahisi isiyokuwa na madhara kwa mtumiaji, pia matibabu yake ni rahisi yenye kumuwezesha kila mwanajamii kumudu gharama, kwani yamekuwa yakiuzwa kwa kwa bei nafuu sana. Baadhi ya madini yanayopatikana katika matango ni Calcium, Phosphorus, Potassium, Zink, Vitamin B, C na E. Madini haya ni muhimu sana katika mwili wa binadamu na yanapopungua au kukosekana mwilini husababisha magonjwa mbalimbali kama magonjwa ya moyo...

KUTAPIKA WAKATI WA UJAUZITO; NANI ASIYE PENDA KUELEWA JAMBO HILI??

Image
Kutapika ni dalili inayojitokeza kwa mama mjamzito hasa kipindi cha awali ingawa tatizo la kutapika au kuhisi kichefuchefu linaweza kutokea katika maradhi mengine mbali na ujauzito. Hali ya kutapika kwa mama mjamzito imegawanyika katika makundi mawili.Kwanza ni kichefuchefu na kutapika wakati wa kipindi cha mwanzo cha ujauzito ( Early pregnancy) na pili ni kipindi baada ya hicho cha awali (Late pregnancy). Tukiingia kiundani kila kundi limegawanyika katika sehemu mbili.Ingawa hatutazama ndani zaidi,ila jambo la msingi ni kwamba katika hali ya awali (Early pregnancy),kutapika na hali ya kichefuchefu inaweza kuwa ya kawaida na isimletee shida kubwa mama (Morning sickness) na kutapika kidogo (emesis Gravidarum) na kuwa mgonjwa hata asiweze kufanya shughuli nyingine. Mama huumwa hadi kuishiwa maji mwilini kwa kutema mate,kutapika na kushindwa kula na wakati mwingine hulazwa hospitali, hali hii huitwa kitalaam “Hyperemesis gravidarum.” Yapo magonjwa mengine yanayosababisha kichefuc...

FAIDA YA MATUMIZI YA TENDE KATIKA KUONGEZA KINGA YA MWILI NA TENDE

Image
TENDE ni chakula chenye hali ya juu ya sukari na huliwa zikiwa mbichi au mbivu. Katika kila gramu 100 (100gm) mna lishe kwa asilimia ifuatayo:- Moisture (Unyevunyevu) 15.3 % Protein (hamirojo) 2.5% Fat (mafuta) 0.4% Carbohydrate (wanga) 75.8% Fibre (kambakamba) 4% Mineral matter (madini) 2.1 % Baada ya funga ya muda mrefu kuanzia alfajiri hadi jioni (magharibi) ni bora kufungua saumu yako kwa kuanza kula tende kwa sababu ni chakula chepesi na husagwa tumboni kwa urahisi. Baada ya huleta nguvu mwilini haraka na pia hulipa tumbo nguvu ya kusaga vyakula vitakavyofuatia baadae. Tende hutofautiana katika ubora kutokana na kutegemea zinatoka nchi gani. Pia hutegemea ikiwa tende hizo ni mpya kutoka shambani au ni za mavuno ya zamani. Tende bora zaidi huwa na faida nyingi za kitiba lakini bei yake ni ghali na tende ya hali ya chini na ya zamani kuvunwa bei yake ni rahisi ukilinganisha na tende mpya lakini faida yake kimatibabu ni ndogo zaidi. Mimi kama Daktari nashau...

DAWA ZA USINGIZI CHANZO CHA SARATANI NA KIFO?

Image
Utafiti uliofanywa nchini Marekani hivi karibuni umetoa matokeo ya kushangaza kwa kusema ya kwamba matumizi ya dawa za usingizi huongeza hatari ya kupata saratani pamoja na mtu kufa mapema. Utafiti huo umesema wale wanaotumia dozi kubwa ya dawa ya usingizi wako kwenye hatari ya kupata magonjwa ya saratani. Utafiti huo ambao ulifanywa na watafiti wa kitengo cha usingizi katika kituo cha Jackson Hole Centre for Preventive Medicine in Wyoming and the Scripps Clinic Viterbi Family Sleep Centre kilichopo jijini California nchini Marekani ili kuangalia hatima ya watu wanaotumia dawa za usingizi aina ya benzodiazepines kama temazepam, diazepam (valium), dawa mpya aina ya zolpidem, zopiclone, zaleplon, dawa za jamii ya barbiturates na zile zinazotumiwa kutibu mcharuko mwili (allergy) na ambazo huleta usingizi. Matokeo ya utafiti huo yanasema wale wanaotumia dawa za usingizi (Hypnotics) walizoandikiwa na Daktari wako kwenye hatari ya 4.6 kufa ndani ya miaka 2 na nusu ukilin...