JE, NI KWELI MATANGO NI DAWA?
MATANGO si matunda mageni katika jamii ya Watanzania kwani hulimwa katika mikoa mbalimbali na mengine kuagizwa kutoka nchi za nje, hivyo kufanya upatikanaji wake uwe mzuri katika masoko ya ndani.
Kihistoria, asili ya matango ni bara la Asia, hasa nchini India. Na matango yalianza kulimwa huko Asia zaidi ya miaka 3000 na baadae zao hilo kusambaa na kupokowa vizuri na nchi za magharibi hasa Ufaransa katika karne ya tisa. Baadae Uingereza na Marekani walianza kulima zao hilo katika karne ya 14 na 16.
Matango yana uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali na kwa njia rahisi isiyokuwa na madhara kwa mtumiaji, pia matibabu yake ni rahisi yenye kumuwezesha kila mwanajamii kumudu gharama, kwani yamekuwa yakiuzwa kwa kwa bei nafuu sana.
Baadhi ya madini yanayopatikana katika matango ni Calcium, Phosphorus, Potassium, Zink, Vitamin B, C na E. Madini haya ni muhimu sana katika mwili wa binadamu na yanapopungua au kukosekana mwilini husababisha magonjwa mbalimbali kama magonjwa ya moyo na saratani.
Faida za tango mwilini
Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida.
Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu. Pia tango linaaminika kupunguza kiwango cha rehemu, mafuta yenye madhara mwilini, huimarisha misuli na pia husaidia usagaji wa chakula tumboni hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa choo.
Virutubisho vilivyopo katika tango hutoa nafuu kawa mtu mwenye matatizo ya ini, kongosho, figo na matatizo katika kibofu cha mkojo.
Watalamu wetu wanatueleza kuwa tango lina kirutubisho kinachojulikana kama ‘erepsin’ ambacho husaidia uzalishaji wa ‘amino acids’ ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa protini mwilini.
Vile vile tango lina kiwango kikubwa cha vitamin C hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yatokanayo na ukosefu wa vitamin hiyo, kama vile fizi kuvuja damu, upunguvu wa damu kwa watoto wachanga na kuota meno na mifupa vibaya.
Kinga ya Saratani
Pengine faida kubwa kuliko zote unazoweza kuzipata kwa kula tango au juisi yake mara kwa mara ni kinga dhidi ya saratani za aina mbalimbali. Jambo hili linalotokana na ukweli kuwa tango lina kiwango kikubwa cha uchachu ‘alkaline’, na kufanya seli za saratani kuwa katika mazingira magumu ya kusambaa mwilini, kwani kwa kawaida seli za saratani haziwezi kuishi kwenye mazingira zenye uchachu.
Hivyo ni vyema kujijengea mazoea ya kula tango mara kawa mara ili kujiwekea ulinzi na kinga ya saratani za aina mbalimbali.
Dawa ya magaonjwa ya ngozi
Tangu enzi na enzi tango limekuwa likitumika katika masuala ya urembo wa ngozi. Watu wengi hutumia tango kwa njia mbalimbali kutunza ngozi zao na kupendezesha sura, hata baadhi ya vipodozi visivyo na madhara hutengenezwa kutokana na tango.
Ulaji wa tango na unjwaji wa juisi yake mara kwa mara huondoa matatizo mengi ya ngozi yaliyo ndani na nje, kama utachukua hatua ya kutumia juisi yake kwa muda wa wiki mbili hadi tatu mfululizo.
Baada ya matumizi, hakika utakuwa na ngozi nyororo yenye afya kushinda mtu anayetumia vipodozi.
Jinsi ya kuandaa juisi ya tango
Ni rahisi sana kutengeneza juisi ya tango. Chukua tango, katakata vipande tayari kwa kusaga ama kwa mashine au kwa kutwanga katika kinu maalumu, kisha changanya na maji masafi ili kupata juisi glasi moja.
Unaweza kuweka sukari kiasi kidogo sana au unaweza kuweka asali kijiko kimoja utapata matokeo mazuri ya haraka kama ukinywa juisi yako asubuhi kabla ya kula kitu chochote.
Ili kutibu matatizo ya ngozi au magonjwa mengine kama tulivyoyaeleza hapo juu, inakupasa kunywa juisi ya tango kwa muda wa wiki mbili au nne mfululizo kisha angalia matokeo yake.
Kwa afya njema, jenga mazoea ya kunywa japo mara mbili au tatu kwa wiki, vilevile unaweza kujiwekea mazoea ya kula tango kwa njia mbalimbali kama vile kuchanganya na saladi, kachumbali au kulitafuna lenyewe mara kwa mara kwani faida zake ni nyingi mwilini.
Makala haya yameandikwa na Felix RM, kwa msaada wa mtandao na vyanzo mbalimbali vya habari.
Comments
Post a Comment